Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, September 30, 2015

MBEYA CITY KUTOA TAMKO KUHUSU NYOSSO BAADA YA SAA 86





WAKATI Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu nchini likiwa  limemfungia mchezaji Juma Nyoso kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi 2,000,000 kufuatia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco, uongozi wa Mbeya City umeagiza Idara ya Mawasiliano na Mahusiano kufanya uchunguzi ndani ya saa 86.

Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo  namba 32 wa Ligi Kuu kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Katika taarifa yake kwa Umma inasema  Bodi ya Mbeya City ilikutana Septemba 29 kwa dharura kulijadili suala ambalo linaendelea kujadiliwa katika Umma wa wanamichezo nchini likimuhusisha mchezaji wa timu yao Juma Said maarufu kama “Nyoso” baada ya mchezo kati ya timu yetu na Azam Fc uliochezwa  27.9.2015 katika uwanja wa Chamanzi.
Katika kikao hicho iliamuliwa kuwa  idara ya Mawasiliano na Mahusiano kulifanyia utafiti suala hili na bodi ikaongezea idara hiyo wajumbe wawili ili kuunda kikosi kazi kitakachofanya kazi kwa adidu za rejea kwa kupitia rejea za mchezo husika na kuangalia mazingira na asili ya suala zima lililojitokeza.
Pia kupata maelezo ya awali ya mchezaji juu ya suala lenyewe na  kufanya uchambuzi wa kisayansi wa mzizi wa suala analohusishwa mchezaji kwa kushirikisha watalaamu wa Ushauri Nasihi na Saikolojia kisha kuishauri Bodi.

Katika taarifa hiyo bodi imeagiza kazi hii iwe imekamilika ndani ya saa 86 kuanzia juzi saa saba mchana ilipoanza.
Pia Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emanuel Kimbe amesema klabu inaomba umma wa wanamichezo kuwa na subira wakati wakiendelea kufanya uchunguzi wa suala hilo

No comments:

Post a Comment