MABONDIA Thomas Mashali na
Francis Cheka watapanda ulingoni Desemba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro katika pambano lisilo la ubingwa.
Pambano hili lisilokuwa na ubingwa litakuwa
la raundi 12.Akizungumzia pambano hilo promota Kaike Siraju alisema kuwa mabondia hao wamesaini mkataba wa kupigana kwenye pambano hilo mbele ya wakili Paul Kalomo wa Dar es Salaam.
“Ni kweli nimeandaa pambano kati ya Cheka na Mashali ambalo litachezwa Siku ya Christimas kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro na maandalizi yanaenda vizuri kwani mabondia wameshaingia makubaliano kwa kusaini mbele ya wakili kwani sitaki ubabaishaji”, alisema Siraju
Pia Siraju alisema kutakuwepo na mapambano ya utangulizi na ulinzi ni wa kutosha siku hiyo hivyo wakazi wa Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Iringa Dodoma na Tanga na wapenzi wote wa ngumi mnaombwa kufika kujionea pambano hilo.
Katika pambano la utangulizi Vicent Mbilinyi atapigana na Deo Njiku huku Cosmas Cheka ambaye ni mdogo wake na Francis Cheka akimfundisha ngumi Mohamed ambaye pia anatoka kwenye familia ya ngumi.
Mapambano ya utangulizi yatakuwa ya raundi sita.
No comments:
Post a Comment