Pages

Tuesday, September 1, 2015

LIVERPOOL YAMUUZA FABIO BORINI

Liverpool wameikubali Ofa ya Pauni Milioni 10 kumnunua Mchezaji wa Kimataifa wa Italy Fabio Borini.
Borini, mwenye Miaka 24, aliichezea Sunderland kwa Mkopo katika Msimu wa 2013/14 na kuifungia Bao 7 katika Mechi 32.
Borini amekuwa pia akisakwa na Inter Milan, Fiorentina na Watford lakini hakuna hata mmoja aliefikia Dau ambalo Liverpool walikuwa wakilitaka.
Borini ndie alikuwa Mchezaji wa kwanza kabisa kwa Meneja Brendan Rodgers kumsaini mara tu aliposhika wadhifa wake Klabuni Liverpool kwa kumnunua kutoka AS Roma Julai 2012 kwa Dau la Pauni Milioni 11.
Akiwa na Liverpool, Borini amefunga Bao 3 katika Mechi 38.

No comments:

Post a Comment