Pages

Tuesday, September 1, 2015

CHELSEA YAMSAINI BEKI MSENEGALI, PAPY DJILOBODJI.

Chelsea wapo njiani kumsaini Beki wa Kimataifa wa Senegal Papy Djilobodji kutoka Nantes ya France kwa Dili ya Pauni Milioni 4.
Tayari Klabu hizo mbili zimeshakubaliani Dili ya Uhamisho ya Beki huyo mwenye Miaka 26 ambae ni chaguo la pili la Jose Mourinho baada ya kumkosa Sentahafu wa Everton John Stones.
Djilobodji, mwenye Urefu wa Futi 6 Inchi 4, ameichezea Nantes Mechi 160 tangu ajiunge nao Mwaka 2010.
Mourinho ameamua kuimarisha Difensi yake baada ya kujikuta wako Pointi 8 nyuma ya Vinara Man City kwenye Ligi Kuu England na Mechi inayofuata kwao ni huko Goodison Park hapo Septemba 12 dhidi ya Everton.
Wakati huo huo Winga wa Nigeria Victor Moses, mwenye Miaka 24, anatarajiwa kusaini Mkataba mpya na Chelsea lakini atapelekwa West Ham kwa Mkopo.
Moses amekuwa nje ya Chelsea kwa Misimu Miwili iliyopita akicheza kwa Mkopo huko Liverpool na Stoke mara tu baada ya kujiunga kutoka Wigan Mwaka 2012 kwa Dau la Pauni Milioni 9.

No comments:

Post a Comment