Pages

Saturday, August 29, 2015

ADIDAS YAWEKA WAZI JEZI MPYA ZA MAN UNITED, NI KAMA JEZI ZA ENZI ZA 1990

BAADA ya Jana Usiku kufanikiwa kutinga Hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kuitwanga Ugenini Club Brugge ya Belgium 4-0 na kuitoa kwa Jumla ya Bao 7-1 katika Mechi mbili, Manchester United Leo wameanua Jezi zao mpya za tatu kwa ajili ya Msimu huu mpya.
Jezi hizo zilizotengenezwa na Adidas ni Rangi Nyeusi zikiwa na Mistari Mekundu na ni mahsusi kwa kutumiwa Mechi za Ugenini za UEFA CHAMPIONS LIGI.Mara ya mwisho kwa Man United kutumia Jezi Nyeusi ni Mwaka 1993 na Bukta za Jezi hizi mpya zimefuata urembo wa Jezi zao za Mwaka 1990 kama alivyovaa Pichani Meneja Msaidizi wao Ryan Giggs wakati akiwa Mchezaji.
Man United walianua Jezi zao za Adidas Nyekundu za Mechi za Nyumbani Old Trafford hapo Agosti Mosi ambayo ni Siku rasmi kwa Mkataba wao wa Pauni Milioni 750 na Adidas kuanza rasmi.
Agosti 11, Man United walianua Jezi zao za Mechi za Ugenini ambazo ni Nyeupe na Bukta Nyeusi. Jumapili Man United wako Ugenini huko Liberty Stadium kucheza na Swansea City katika Mechi ya Ligi Kuu England.Juan Mata

No comments:

Post a Comment