Pages

Saturday, September 19, 2015

BAADA YA KUFUNGA MABAO MAWILI KIIZA AGOMA KUTOA AHADI SIMBA



 Hamisi Kiiza, mshambuliaji wa klabu ya Simba
PAMOJA na kuanza vema ligi huku akiwa amefunga mabao mawili, Hamis Kiiza amesema hawezi kusema hayo ni mafanikio.
Kiiza ambaye anachezea Simba msimu huu baada ya Yanga kumwacha msimu uliopita amefanikiwa kufunga mabao mawili kwenye uwanja wa Mkwakwani jambo linalotafisiriwa kuwa Simba imevunja mwiko kwani ilizoeleka kupoteza mechi kwenye uwanja huo.
“Nashukuru timu imeanza vizuri kitu ambacho ni kizuri kwa sisi wachezaji na wapenzi wa Simba lakini bado hatuwezi kusema haya ni mafanikio bado tunataka kuendelea kufanya vizuri na tunapofanya vizuri kila kitu atafurahi”, alisema Kiiza
Pia Kiiza alisema Simba kuna umoja kwani kwenye timu kila mmoja anajituma na anajua umuhimu wa ushindi
Kiiza alisema kila timu wanayocheza nayo wanaiheshimu kwani wanajua kila timu ni ngumu na wao wanakwenda kwa ugumu ili wapate matokeo mazuri, kiujumla tunafanya vizuri kwasababu ya ‘team work’ tunapendana wote.
Pamoja na kuanza vizuri lakini ameshindwa kuahidi kuwa atafunga mabao mangapi ila alisema anataka kuisaidia timu yake kufanya vizuri, kupata pointi tatu hata kama hajafunga anaweza kutengeneza watu wakafunga wakapata ushindi lakini sio Kiiza kuibuka mfungaji bora na timu haijachukua ubingwa.
Kiiza alisema timu ni sehemu yake ya kazi na yeye anaheshimu kazi anapokuwa kazini na kusema alivyokuwa Yanga, alikuwa anaipenda kazi yake ndio maana alifanikiwa na sasa hivi yupo Simba anafanya vizuri anaipenda kazi yake ndio maana ametulia kwani amekuja Tanzania kufanya kazi, hajaja kufanya mapenzi.

No comments:

Post a Comment