Pages

Saturday, September 19, 2015

Miaka 17 ya Kituo cha Mazoezi cha Home Gym: kutembelea wodi ya wazazi Kituo cha Afya Sinza Palestina leo Sept 19

home gym

Kituo cha Mazoezi cha Home Gym…

Na Andrew Chale, modewjiblog
[Dar es Salaam-Tanzania]- Kuelekea miaka 17 ya tangu kuanzishwa kwa  kituo cha Mazoezi cha Home Gym chenye maskani yake Mwenge jijini Dar es Salaam-Tanzania, uongozi wa kituo hicho unatarajia kufanya matukio makuu muhimu ikiwemo kutembelea  wodi ya akina mama katika kituo cha Afrya cha Sinza Palestina Jijini.
Akizungumza na modewjiblog, Mkurugenzi wa kituo hicho, Andrew Mangomango amebainisha kuwa, kuelekea shughuli za miaka 17 za tangu kuanzishwa kwake kituo hicho, hiyo Septemba 20,  siku  moja kabla yaani leo  Septemba 19, watafanya tukio la kufariji wagonja kwenye kituo cha afya cha Sinza Palestina ambapo pia watatoa zawadi mbalimbali kwa walengwa akina mama pamoja na zoezi la ufanyaji usafi.
“Septemba 19, uongozi wa wadau wote tutatembelea kituo cha Afya cha Sinza Palestina na kufariji wagonja katika wodi ya wazazi. Hii ni pamoja na kutoa vitu muhimu vinavyowakabili wazazi hasa katika masuala mazima ya uzazi.” Amesema Andrew Mangomango.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa, kutokana na mazoezi ni afya, hivyo wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuakikisha wanasaidia afya za watu wote hapa nchini ikiwemo kuimalisha miili yao kupitia mazoezi mbalimbali hasa ya viungo.
Aidha, katika upande wa shughuli ya Septemba 20 yaani kesho, ambayo watakuwa wakisheherekea miaka hyo 17, tangu kuanzishwa kwa Home gym,   wanatarajia watu zaidi ya 500, kushiriki katika Bonanza hilo.
Zoezi hilo linataraiwa kuhusisha vikundi mbalimbali vya jogging, vituo vya gym mbalimbali  siku ya juma pili hii ya septemba 20 katika viwanja vya Escape One.
Andrew Mangomango  anabainisha kuwa,  zoezi hilo litaanzia Mlimani City majira ya saa kumi na mbili asubuhi kwa washiriki kukimbia kwa mwendo wa taratibu pamoja na kutembea kwa makundi  na kuishia viwanja vya Escape One.
Ratiba ya Bonanza:
Baada ya kuwasili katika viwanja  vya Escape One,  saa mbili asubuhi itaanza AEROBICS mpaka saa nne asubuhi na mara baada ya hapo kutakuwa na michezo mbalimbali  ikiwemo  kuvuta Kamba, kukimbia na magunia, kukimbiza kuku kunyanyua vitu vizito , kutunisha misuli, mpira wa miguu pamoja na Burudani ya muziki,  lakini pia kutakuwa na michezo mbalimbali kwa watoto hivyo kuwataka wazazi kwenda na watoto wao ili kufurahia kwa pamoja.
Bonanza hilo limebeba kauli mbiu isemayo FANYA MAZOEZI KWA AFYA YAKO likiwa na lengo la kuwahamasisha watu wote kushiriki katika mazoezi ili kutunza afya zao.
Kituo hicho cha mazoezi kilichoanzishwa mwaka 1998  kimekuwa na mchango mkubwa katika kujenga na kulinda afya za watu wengi kupitia mazoezi mbalimbali yanayotolewa kwenye kituo hicho kwa kipindi chote.
gym
Moja ya matukio ya Bonanza la mazoezi la kityuo hicho cha Home Gym (picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi)
home-gym-entertainment
Baadhi ya vifaa vya kisasa kabisa vya mazoezi katika kuimalisha mwili ambapo Home gym wanayatoa pia kwa watu mbalimbali kwenye kituo chao hicho cha mazoezi, Mwenge jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment