YANGA YATUMA SALAMU SIMBA BAADA YA KUIFUNGA JKT RUVU 4-1
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga jana waliendelea
kutoa dozi katika ligi hiyo baada ya kuwafunga maafande wa JKT Ruvu kwa mabao
4-1 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Ushindi
huo ni kama inawatishia nyau wapinzani wao wa jadi Simba, ambayo itacheza nao
mwishoni mwa wiki ijayo kwenye uwanja huo.
Huo
ni mchezo wa tatu mfululizo kwa timu hiyo yenye maskani yake Jangwani kushinda
na kuifanya kujikusanyia pointi tisa na mabao ya kufunga tisa huku ikiwa
imefungwa bao moja tu hadi sasa.
Yanga
walianza kwa kasi mchezo wao huo dhidi ya JKT Ruvu baada ya kulishambulia lango
la wapinzani wao katika dakika ya kwanza tangu kuanza kwa mchezo huo, lakini
Donald Ngoma alipiga shuti lililogonga mwamba na kurudi uwanjani baada ya pasi
nzuri ya Niyonzima.
Katika
dakika ya 21, Yanga nusura wafunge lakini shuti la Thaban Kamusoko la mpira wa
adhabu liligonga mwamba na kutoka nje.
Baada
ya kushambulia mfululizo, Yanga walifanikiwa kupata bao la kuongoza katika
dakika ya 34, mfungaji akiwa ni Mzimbabwe Donald Ngoma kwa shuti la mbali akimalizia pasi ya Amiss
Tambwe.
Mrundi
Tambwe aliifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 47 baada ya kumalizia
mpira uliotemwa na kipa wa JKT Ruvu.
Dakika
mbili baadaye JKT Ruvu walijitutumua na kupata bao lililofungwa na Michael
Aidan.
Tambwe
aliendelea kuwa mwiba mchungu kwa maafande hao wa JKT Ruvu baada ya kufunga kwa
kichwa bao la tatu katika dakika ya 62, akiunganisha wavuni kwa kichwa mpira wa
kona iliyochongwa na Simon Msuva.
Msuva
nusura aipatie Yanga bao la nne katika dakika ya 70 baada ya shuti lake akiwa
ndani ya eneo la hatari kupanguliwa na kipa wa JKT Ruvu na kuwa kona ambayo
haikuzaa matunda.
Kiungo
mpya wa Yanga, Thabani Kamusoko aliifungia timu yake hiyo bao la nne na
kuihakikishia kuondoka na pointi zote tatu baada ya kupiga shuti kali la mbali
lililojaa wavuni.
Yanga:
Ally Mustapha, Mbuyu Twitte, Haji Mwinyi, Kelvin Yondan, Nadir Haroub, Thaban
kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Salum Telela, Amiss Tambwe, Donald
Ngoma/Malimi Busungu na Deus Kaseke, Geofrey Mwashiuya.
JKT
Ruvu:Tony Kavishe, Michael Aidan, Napho Zuber, Martin Kazila, Madenge
Ramadhani, George Minja, Ismail Azizi/Gaudence Mwaikimba, Naftali Nashon,
Samuel Kamuntu/Abdul Mussa, Saady Kipanga/Emmanuel Pius na Mussa Juma.
Katika
mechi zingine jana Jumamosi, Stand United iliifunga African Sports ya Tanga kwa
mabao 2-0, Mgambo Shooting iliitambia Majimaji ya songea 1-0 na Prisons iliwatuliza ndugu zao wa Mbeya
City kwa kuwafunga bao 1-0.
No comments:
Post a Comment