Pages

Tuesday, September 22, 2015

ASHANTI UNITED YAANZA KWA KIPIGO LIGI DARAJA LA KWANZA

TIMU ya soka ya kiluvya United ‘Wabishi wa Pwani’ juzi walianza vema kivumbi cha ligi daraja la kwanza baada ya kuichapa timu ya Ashanti united ya Jijini Dar es  salaama kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa mabatini Mlandizi.
 
Mchezo huo wa ligi daraja la kwanza ulikuwa na ushindani mkali kutokana na timu zote mbili kucheza mpira wa kasi katika dakika za kipindi cha kwanza kwa lengo la kuweza kuondoka na ushindi na kujinyakulia pointi tatu muhimu  lakini hadi hadi mapumziko hakuna mbambe aliweza kuzifumania nyavu za mwenzake.
 
Kipindi cha pili timu ya Kiluvia United ilionekana kuingia kwa kubadilisha mfumo wa mashambulizi na kuanza kulisakama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kuandika bao la kwanza kunako katika dakika ya 47 lililowekwa kimiani na mshsambuliji wao wa kutumaniniwa Chala Juma.
 
Kuingia kwa bao hilo kuliweza kulionekana kuwachanganya wachezaji wa Ashanti United kwa kujipanga upya na kujaribu kuongeza kasi zaidi kwa lengo la kupata bao la kusawazisha lakini kutokana na safu ya ulinzi ya Kiluvya United kuwa imara waliweza kuthibiti mashambulizi ya wapinzani wao.
 
Mchezaji Kulwa Muanda pamoja na kimo chake kuwa ni kifupi aliweza kuonyesha uwezo wake katika kulisakata kabumbu baada ya kuwainua mashambiki wa kiluvva united baada ya kupachika bao la pili baada ya kuiunganisha krosi safi iliyochongwa Chala Juma na kuwamwacha mlinda mlango wa Ashanti United amebaki mdomo wazi.
 
Ashanti United licha ya kuwahi kuonja joto la kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara walijikuta wanakabwa koo na wabishi hao wa Pwani na kupelekea hadi kipenga cha dakika tisini kinapulizwa timu ya Kilivya ilitoka uwanjani hapo kifua mbele kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzania wao.
 
Mara baada ya kumalizika kwa matanange huo mlezi wa timu hiyo Edward Mgogo almaarufu (Eddo Master) alisema kwamba vijana wake  wameonyesha mchezo mzuri na kupatikana na ushindi huo ni kutokana na kujituma katika dakika zote za mchezo huo.
 
 Aidha Eddo alisema kwamba ana imani vijana wake wataweza kufika mbali na kufanya vizuri katika ligi daraja la kwanza na kuwaomba wadau wa Mkoa wa Pwani mchezo wa kandanda  kwa ujumla sambamaba na wana kiluvya wote kuhakikisha wanaipa  ushirikiano wa dhati timu hiyo katika ligi hiyo ya daraja la kwanza amabyo inaushindani mkubwa kutokana na kuzishirikisha timu amabzo zilishawahi kushiriki ligi kuu ya Tanzania bara.
 

No comments:

Post a Comment