Pages

Tuesday, September 22, 2015

ILALA MABINGWA WAPYA WA AIRTEL RISING STARS


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi jana amefunga fainali za michuano ya kombe la Airtel Rising Stars katika uwanja Karume jijini Dar es salaam.
Akiongea wakati wa ufungaji michuano ya Airtel mbele ya halaiki ya vijana walioshirki michuano hiyo, Malinzi ameishukuru kampuni ya simu ya Airtel kwa kuendelea kudhamini michuano hiyo ambayo inawapa nafasi vijana ya kucheza mpira na kuonekana na baadae kujipatia ajira.
“Lengo la TFF ni kushirki fainali za Olimpiki za Dunia mwaka 2020 Tokyo –Japan hivyo wachezaji wenye vipaji kutoka kwenye michuano hii ya Airtel na vijana wengine wataendelea kutunzwa kwa ajili ya timu ya Taifa ya baadae” Alisema Malinzi.
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ambao ndio wadhamini wakuu wa michuano hiyo, amesema airtel wataendelea na program hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kwa wanawake na wanaume, na kuahidi kuendelea koboresha michuano hiyo kila mwaka.
Michuano ya Airtel Rising Stars ilizisihirkisha timu za wanaume na wanawake kutoka mikoa saba nchini, huku mashindano hayo yakiwa yanafanyika kwa msimu wa tano sasa tangu kuanzishwa mwaka 2011.
Kwa upande wa wanaume, timu ya Ilala imeibuka mabingwa baada ya kuifunga Mbeya kwa mabao 4-0 katika mchezo wa fainali ulochezewa jioni, huku timu ya wanawake ya Temeke wakiibuka washindi baaada ya kuibwaga Kinondoni mwa mikwaju ya penati 5-4.

No comments:

Post a Comment