Ligi kuu England Leo imeanza rasmi Msimu wake mpya wa 2015/16 huko Old Trafford Jijini Manchester na Wenyeji Manchester United kuibuka na ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Tottenham Hotspur.
Man United hii Leo iliwatumia Wachezaji wake wanne wapya kuanza Mechi hii ambao ni Kipa Sergio Romero, Matteo Darmian, Morgan Schneiderlin na Memphis Depay na kisha walimuingiza Bastian Schweinsteiger kumbadili Michael Carrick.
Dakika ya 22 Beki wa Spurs Kyle Walker alijifunga mwenyewe katika harakati za kuokoa wakati Kepteni Wayne Rooney akijiandaa kupiga na kuipa Man United uongozi wa Bao 1-0.
Bao hilo lilidumu hadi mwisho wa mchezo.
Mechi inayofuata ya Ligi kwa Man United ni Ijumaa ijayo Ugenini Villa Park watakapocheza na Aston Villa.
Depay akifurahia kwenye mtanange wa leo wa mechi ya kwanza na msimu mpya wa 2015/2016Baadhi ya Wachezaji wa Man United wakipongezana baada ya kupata zawadi ya bao lililoshinikizwa na Wayne Rooney kipindi cha kwanza.De Gea akiwa nje! akiuangalizia benchi na kipa mwenzakeDepay akichuana vikali mpira wa kichwa dhidi ya Eric DierDepay akimisha mpira kwenye eneo la hatariBastian akisisitiza jambo baada ya kuingia kipindi cha piliEric Dier akimvuta jezi Ander HerreraYoung na Walker walitofautiana kidogo hapaVan Gaal Wayne Rooney alionekana kavaa kitambaa cheuzi mkononi kutokana na kumbukumbu kifo cha Mzee Garry na Phil1-0, Mpaka mapumziko Man United walienda wakiwa mbele ya bao hilo moja la kujifunga. Spurs walijitahidi kushambulia kipindi cha kwanza lakini hawakubahatika kupata bao.Kyle Walker dakika ya 22 anajifunga na kuipa zawadi ya bao Man United baada ya Rooney kuchelewa kufunga bao.Kipa Romero kaanza
Mtanange umeanza kipindi cha kwanza...0-0VIKOSI:
Manchester United (4-3-3): Romero; Darmian, Smalling, Blind, Shaw; Carrick, Memphis, Schneiderlin; Mata, Rooney, Young.
Subs: Johnstone, Valencia, McNair, Schweinsteiger, Herrera, Pereira, Hernandez.
Tottenham (4-2-3-1): Vorm; Walker, Alderweireld, Vertonghen, Davies; Bentaleb, Dier; Chadli, Eriksen, Dembele; Kane.
Subs: Johnstone, Valencia, McNair, Schweinsteiger, Herrera, Pereira, Hernandez.
Tottenham (4-2-3-1): Vorm; Walker, Alderweireld, Vertonghen, Davies; Bentaleb, Dier; Chadli, Eriksen, Dembele; Kane.
No comments:
Post a Comment