Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 8, 2015

AWADHI AWAPA RAHA MASHABIKI WA SIMBA








BAO la dakika ya 90 la Awadh Juma liliwezesha Simba kuibuka na pointi tatu kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya SC Villa ya Uganda uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya Simba Day.

Awadh ambaye aliingia kwenye mchezo huo akitokea benchi kuchukua nafasi ya  Justuce Majivba alifunga bao hilo kwa shuti baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la Villa.

Ushindi huo umenogesha tamasha hilo la Simba Day ambalo hufanyika kila mwaka kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tamasha hilo pia lilitumika kuwatambulisha wachezaji wapya wa Simba ambao wamesajiliwa msimu huu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.

Katika mchezo huo, Simba ilianza kwa kulishambulia lango la Villa, lakini umakini wa mabeki wake waliweza kuzuia mashambulizi langoni mwao na hivyo kuufanya mchezo huo kusubiri hadi dakika ya 90 kuweza kubadilisha matokeo ya suluhu.

Wachezaji wapya waliotambulishwa kwenye mchezo huo ni pamoja na Emery Nimubona, Justice Majivba, Hamis Kiiza na Mwinyi Kazimoto ambaye awali aliichezea timu hiyo kabla ya kutimkia Uarabuni kucheza soka la kulipwa.

Tamasha hilo lilinogeshwa na burudani mbalimbali, ambapo awali ulianza mchezo kati ya viongozi wa Simba na wasanii wa Bongo fleva na Bongo muvi ambao ni mashabiki wa Simba.

Kwenye mchezo huo, viongozi wa Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na kocha, Dylan Kerr.

No comments:

Post a Comment