Pages

Wednesday, August 19, 2015

UCHAGUZI TEFA AGOSTI 23, YAANI JUMAPILI



KAMATI ya uchaguzi ya Chama cha Soka mkoa wa Dar es Salaam, (DRFA) imeitaka kamati ya uchaguzi ya TEFA kufanya uchaguzi wa viongozi, Agosti 23, kama ilivyopangwa
Akizungumza na wandishi wa habari, msemaji wa DRFA, Omar Katanga alisema awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike jumapili iliyopita katika ukumbi wa JKT Mgulani lakini uliahirishwa wanachama wakiwa ukumbini.
“Kamati inapenda  kuutarifu umma kuwa mchakato wa ucaguzi una baraka zote kutoka TFF, hivyo uingiliaji wowote unakwenda kinyume na ibara ya 6(1)ya kanuni za uchaguzi za TFF 2013 na ibara za 52(6) na 56(6)(a) za katiba ya TFF ambazo zinaelekeza kuwa majukumu ya uchaguzi yapo chini ya kamati ya uchaguzi”, alisema Katanga.
Itakumbukwa uchaguzi huo uliokuwa ufanyike jumapili iliyopita na uliahirishwa na kamati ya uchaguzi ya Tefa licha ya TFF kuagiza ufanyike hivyo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi DRFA wakili, Rashid Saadallah akaitaka kamati hiyo ya TEFA kumuandikia barua kueleza sababu ya kuahirisha uchaguzi huo.
baada ya kupitia sababu hizo,ndipo DRFA ikatoa majibu kwa kuelekeza uchaguzi huo kufanyika jumapili hii.
Pia Katanga alisema kozi ya ukocha leseni C inatarajiwa kufanyika kuanza Agosti 28, katika ukumbi wa TFF, Uwanja wa Karume na washiriki wanakumbushwa kulipia ada za ushiriki ambayo ni shilingi  250,000.

No comments:

Post a Comment