Pages

Wednesday, August 19, 2015

KOMBE LA TFF KUSHIRIKISHA TIMU 60, BINGWA KUCHEZA KOMBE LA SHIRIKISHO



JUMLA ya timu 60 zinatarajiwa kuoneshana umwamba kwenye kombe la chama cha soka nchini linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba mwaka huu.
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Baraka Kizuguto alisema kombe hilo ambalo ni maarufu kama kombe la Shirikisho litazikutanisha timu zinazocheza ligi daraja la pili, daraja la kwanza na ligi kuu.
“Kombe la shirikisho litachezwa kwa mtindo wa mtoano na bingwa ndiye atawakilisha nchi kwenye kombe la shirikisho barani Afrika”, alisema Kizuguto
Pia endapo itatokea bingwa wa kombe la Shirikisho akaibuka bingwa ligi kuu basi mshindi wa pili wa kombe la shirikisho ndie atachukuliwa kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kombe la shirikisho ambalo misimu iliyopita mshindi namba mbili wa ligi kuu ndiye alikuwa anaiwakilisha nchi.
Timu zitakazo shiriki ni 16 ambazo zinacheza ligi kuu na 24 za daraja la kwanza na 24 pia zinazocheza ligi daraja la pili.
Pia amezivitaka klabu zote kujiandaa vizuri kwani ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa mtoano.
Kizuguto alimalizia kusema TFF inavisisitiza vilabu kukamilisha usajili wa wachezaji na viongozi kabla ya kufungwa kwa dirisha leo saa sita usiku kwani baada ya kufungwa kwa usajili hakutakua na muda tena wa nyongeza.

No comments:

Post a Comment