Pages

Wednesday, August 19, 2015

AZAM KUWAKOSA WANGA NA BALOU



WACHEZAJI wawili tegemeo wa Azam FC watakosa mchezo wa ngao ya hisani dhidi ya Yanga utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Msemaji wa Azam FC, Jafar Maganga aliwataja wachezaji hao kuwa ni Mkenya Allan Wanga na Kipre Balou
“Wanga amekwenda kumzika mama yake mzazi ambaye atazikwa siku hiyo ambayo ndio tunacheza na Balou ni majeruhi”, alisema Maganga
Kiungo huyo Mshambulizi ambaye amesajilwa Azam FC akitokea El Marrekh  ya Sudan amekuwa mwiba mchungu kwa timu pinzani pindi wakicheza hata Azam FC hawatamsahau kwani ndiye aliyefunga bao la tatu lililoiondoa kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika
Mchezo wa ngao ya hisani ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la Ligi Kuu  utaanza kutimua vumbi majira ya saa 10 kamili.
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Israel Nkongo, (Dsm), akisaidiwa na Samwel Mpenzu (Arusha), Josephat Bulali (Tanga) na mwamuzi wa akiba ni Hashim Abdallah (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo ni Deogratius Rwechungura kutoka  Mara.

No comments:

Post a Comment