Pages

Saturday, August 22, 2015

TAMASHA LA AMANI KUZURU MIKOA KUMI


Mkurugenzi wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu, Alex Msama akiongea na wandishi wa  habari tamasha hilo ambalo litafanyika Dar es Salaam kwenye uwanja wa Taifa,  Oktoba 4 na baadae kwenye mikoani. Kulia ni Katibu wa kamati hiyo  Khamis Pembe


KAMPUNI  inayoandaa Tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka, imetaja mikoa itakayoomba amani kuelekea uchaguzi Mkuu.

 Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema tamasha hilo kabla ya kuelekea mikoani,  litaanzia jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa Taifa, litakalofanyika Oktoba 4 jijini humo.

Msama  alisema  itikadi  za  vyama  vya  siasa  ni  nyingi  ni lazima tuwe na umoja ili kuzungumzia suala hilo ambalo Mataifa mbalimbali duniani hawana amani hasa katika vipindi vya uchaguzi.
Msama alisema tuweke tofauti  zetu pembeni na kumkimbilia Mungu atupitishe kwa amani katika kipindi cha uchaguzi Mkuu.

Aidha Msama alisema kuelekea uchaguzi Mkuu waimbaji, Boniface Mwaitege na Christopher Mwahangila  wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo huku Kamati ya maandalizi ikiendelea na taratibu za kufanikisha tamasha hilo.

Kauli mbiu ya tamasha hilo  ni Tanzania ni ya kwetu, Tuilinde na kudumu  amani ya nchi yetu ambayo inachochea kufikisha ujumbe wa neno la Mungu.

Msaa aliitaja baadhi ya mikoa itakayofikiwa na tamasha hilo ni pamoja na Morogoro, Iringa, Dodoma, Mbeya, Shinyanga na Mwanza.

No comments:

Post a Comment