MAN U YABANWA NA NEWCASTLE LEO
TIMU ya Manchester United leo imetoka suluhu na
Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliofanyika kwenye Uwanja
wa Old Trafford.
Bao lililofungwa na Wayney Rooney lilikataliwa na mwamuzi kwa madai kuwa
mfungaji alikuwa ameotea baada ya kuwa nyuma ya mabeki wa Newcastle United.
Aleksandar Mitrovic, akicheza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha
Newcastle, nusura aipatie bao timu hiyo baada ya kupiga shuti lililogonga
mwamba kabla ya Javier Hernandez mpira wake kuzuiwa na Krul na Chris Smalling
kugonga mwamba katika muda wa majeruhi.
Matokeo hayo yana maana kuwa wenyeji Man United bado hawajafungwa na
hawajaruhusu bao lolote kutinga katika wavu wao katika mechi za ligi msimu huu.
Louis van Gaal alimuanzisha Schweinsteiger, ambaye baadaye alitoka na
nafasi yake kuchukuliwa na Michael Carrick wakati Newcastle ilifanya mabadiliko
mara tatu kutoka katika kikosi kilichoifunga Swansea.
No comments:
Post a Comment