TIMU
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeanza mazoezi katika Uwanja wa Karume
kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya
Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.
Wachezaji
wa Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa watakuwa wakijifua mara
mbili kwa katika Uwanja wa Karume katika kujiweka sawa na maandalizi ya mchezo
huo.
Kufuatia
baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu na timu zao kujiandaa na mchezo wa Ngao ya
Hisani utakaochezwa Agosti 22, Mkwasa amewaongeza wachezaji wengine kumi (10)
kutoka katika orodha yake ya akiba.
Lengo
la kambi hii ya awali ya siku tano, ni kupata nafasi ya kuwaona wachezaji
katika mazoezi hayo kabla ya safari ya kuelekea nchini Uturuki Agosti 23 mwaka
huu kwa kambi ya siku kumi.
Wachezaji
walioitwa na kuanza mazoezi ni Said Mohamed, Vicent Andrew (Mtibwa Sugar),
Mohamed Hussein, Ibrajim Ajibu (Simba SC), Hamis Ali, Juma Mbwana (KMKM), Tumba
Sued (Coastal Unioni), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ibrahim Hilka (Zimamoto–
Zanzibar) na Mohamed Yusuf (Prisons).
Wachezaji
wengine waliopo kambini ni Said Ndemla, Hassan Isihaka, Abdi Banda(Simba SC),
Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Orgeness Mollel
(Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi (Mafunzo).
No comments:
Post a Comment