Pages

Wednesday, August 19, 2015

KUZIONA YANGA NA AZAM JUMAMOSI 7000



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Azam FC dhidi ya Yanga utachezwa jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salam
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto, alisema mchezo huo ambao ni sehemu ya ufunguzi wa pazi la Ligi Kuu  utaanza kutimua vumbi majira ya saa 10 kamili.
“Mchezo wa Ngao ya Hisani ambao utachezwa jumamosi,kiingilio cha chini kitakuwa ni shilingi elfu saba naVIP A ni 30,000 na tiketi zitaanza kuuzwa siku hiyo ya jumamosi asubuhi katika ya Uwanja wa Taifa”, alisema Kizuguto
Viingilio vya mchezo huo ni 7,000 kwa majukwaa yenye rangi ya kijani, bluu na rangi ya chungwa, VIP B & C ni 20,000 na VIP A ni 30,000.
 Pia alisema tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya mchezo saa 2 kamili katika viunga vya maeneo ya uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo huo utachezeshwa na mwamuzi Israel Nkongo, (Dsm), akisaidiwa na Samwel Mpenzu (Arusha), Josephat Bulali (Tanga) na mwamuzi wa akiba ni Hashim Abdallah (Dsm) wakati kamisaa wa mchezo huo ni Deogratius Rwechungura kutoka  Mara.

No comments:

Post a Comment