Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 8, 2015

DAVID DE GEA AKATWA MAN UNITED, SERGIO ROMERO AU JOHNSTONE KULIONA LANGO OLD TRAFFORD

www.bukobasports.comKipa wa Manchester United David De Gea hatacheza dhidi ya Tottenham hapo Kesho huku akiendelea kuhusishwa na kuhamia Real Madrid.
Kwa kipindi chote hiki kuelekea Msimu mpya ambao unaanza Kesho kwa hiyo Mechi Uwanjani Old Trafford, De Gea, mwenye Miaka 24, ametajwa sana kutaka kurudi kwao Spain kuichezea Real.

Akiongelea Mechi hii ya kwanza, Meneja wa Man United, Louis van Gaal, amesema: “Namfikiria yeye kama binadamu na si Mchezaji. Naona hatamudu haya.”
Kukosekana kwa De Gea kunaweza kufungua njia kwa Kipa mpya wa Kimataifa wa Argentina, Sergio Ramos, kucheza Mechi yake ya kwanza kabisa.
Kipa mwingine wa Man United ni Kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes, mwenye Miaka 33, lakini nae ametemwa kwenye Kikosi cha Kwanza na yumo kwenye Listi ya Wachezaji wanaouzwa baada ya kufarakana na Van Gaal.


Makipa Sergio Romero na De Gea

No comments:

Post a Comment