Pages

Saturday, July 11, 2015

UHAMISHO: ANGELO OGBONNA ASAJILIWA NA KLABU YA WEST HAM UNITED YA ENGLAND

West Ham United imemsaini Sentahafu wa Italy Angelo Ogbonna kutoka Juventus kwa Dau linalotajwa kuwa Pauni Milioni 10.
Ogbonna, mwenye Miaka 27 na ambae ameichezea Italy mara 10, amesaini Mkataba wa Miaka Minne na West Ham.
Msimu uliopita, Ogbonna, ambae alihamia Juve kutoka kwa Mahasimu wao Torino Mwaka 2013, aliichezea Juve Mechi 31.
Ogbonna anakuwa Mchezaji wa 5 kusainiwa na West Ham chini ya Meneja mpya Slaven Bilic na wengine ni Pedro Obiang, Dmitri Payet, Darren Randolph na Stephen Hendrie
Amesaini mkataba wa miaka 4 na West Ham United.

No comments:

Post a Comment