Pages

Saturday, July 11, 2015

IDRISSA GUEYE ASAINI ASTON VILLA KWA MIAKA 4

Aston Villa imekamilisha Uhamisho wa Kiungo kutoka Lille ya Ufaransa Idrissa Gueye kwa Ada ambayo haikutajwa.
Gueye, Raia wa Senegal mwenye Miaka 25, amesaini Mkataba wa Miaka Minne na Villa.
Gueye aliichezea Lille Mechi 134 na kuiwakilisha Nchi yake mara 18.
Gueye anakuwa Mchezaji wa 3 kuchukuliwa na Villa baada ya Mwezi uliopita kuwasaini Scott Sinclair, Miaka 26, na Micah Richards, wote kutoka Manchester City.

No comments:

Post a Comment