Pages

Saturday, July 11, 2015

BASTIAN SCHWEINSTEIGER KUTUA MANCHESTER UNITED, KUPIMWA AFYA HIVI KARIBUNI!

Kiungo wa Mabingwa wa Germany, Bastian Schweinsteiger, yupo njiani kutua Manchester United baada ya ripoti kutoka Nchini kwao kudai ameafiki kuhamia England.
Gazeti kubwa huko Germany, Bild, limetoboa kuwa Schweinsteiger, ambae amebakiza Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake na Bayern, ameijulisha Klabu yake nia yake ya kusaka changamoto mpya na kuungana tena na Meneja wa Man United Louis van Gaal.
Van Gaal na Schweinsteiger, mwenye Miaka 30, walikuwa pamoja huko Bayern kati ya Miaka 2009 na 2011 wakati Van Gaal alipokuwa Meneja na kuwa na uhusiano mzuri sana.
Bild limeripoti kuwa Schweinsteiger atasaini Mkataba wa Miaka Mitatu na Man United utakaomlipa Pauni 140,000 kwa Wiki na hivi sasa yupo akisubiri kuruka kwenda Jijini Manchester kupimwa Afya na kukamilisha taratibu zote za Uhamisho.
Lakini, kwa mujibu wa Bild, kinachochelewesha hilo ni mvutano wa Ada ya Uhamisho ambayo Bayern wanataka Pauni Milioni 15.
Tangu atue Kocha Pep Guardiola huko Bayern, Schweinsteiger amekuwa nyuma ya chaguo la Viungo kwa Kocha huyo wa zamani wa Barcelona akipitwa na kina Xabi Alonso, David Alaba, Thiago Alcantara na hata Fulbeki Phillip Lahm ambae wakati mwingine huchezeshwa kati.
Maishani mwake mwote, Schweinsteiger amekuwa akiichezea Bayern Munich na pia kuwawakilisha Mabingwa wa Dunia Germany kwa kuwachezea Mechi zaidi ya 100.
Ikiwa Schweinsteiger atasainiwa, yeye atakuwa Mchezaji wa 3 kunaswa na Louis van Gaal katika kipindi hiki kufuatia Memphis Depay na Matteo Darmian ambae ndie amekamilisha upimwaji Afya.

No comments:

Post a Comment