Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia
ametuma salama za pongezi kwa uongozi mpya wa klabu ya Coastal Union
uliochaguliwa mwishoni mwa wiki.
Katika salamu zake kwa
Mwenyekiti mpya wa klabu hiyo Dr. Twaha, Karia amesema anawapa pongezi
wa kuchaguliwa na kupewa heshima hiyo na wanachama wa Coastal Union
katika kuitumikia klabu yao.
“Kikubwa wanachopaswa kufanya kwa
sasa ni kuodokana na makundi ya aina yoyote, na kuifanya Coastal Union
kuwa kitu kimoja na kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom”
alisema Karia.
Aidha Karia amesema, TFF itashirkiana na uongozi mpya katika utendaji wa kazi na kuleta maendeleo katika mpira miguu nchini.
Klabu
ya Coastal Union yenye makazi yake jijini Tanga ilifanya uchaguzi wake
mwishoni mwa wiki na kuwapata viongozi wake wapya, akiwemo mwenyekiti,
makamu mwenyekiti na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment