Pages

Friday, July 10, 2015

RAIS KIKWETE AKIRI VIPIGO VYA STARS VINAVYOMUUMIZA


Na Saleh Ally
Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kwa kiasi gani amekuwa akiumizwa na vipigo mfululizo ambavyo Taifa Stars imekuwa ikivipata.


Kikwete ameyesema hayo wakati akilihutubia bunge la Tanzania mjini Dodoma, leo.

Kikwete amekiri kwamba amekuwa akijisikia vibaya kutokana na Stars kupoteza mechi zake mfululizo hadi yeye kufikia kuamua kutokwenda uwanjani.
“Kila ukienda wanafungwa, mwisho ikafikia nikaona hawa wanataka kusema mimi ndiye nina nuksi, nikaacha kwenda. Hata wakiamua Unguja, nako wanapiga tatu,” alisema na kuwachekesha wabunge.
Lakini baadaye Kikwete aliwataka wahusika akiwa na maana ya TFF kufanya jambo ili kubadilisha hali hiyo ya kuwa na timu inayofungwa kila mara.
“Lazima waliangalie hili na kulifanyia kazi kwa kuwa si sahihi,” alisema Kikwete ambaye itakuwa ni hotuba yake ya mwisho kulihutubia bunge akiwa rais.

Aidha, aliendelea kusisitiza uamuzi wake wa kurejesha michezo mashuleni ulivyorejesha ushindani.
Pia akazungumzia namna muziki na sanaa ya uigizaji inavyopaswa kupewa nafasi kwa kuwa wakati mwingine fani hizo zimekuwa zikiwaliwaza Watanzania kimataifa kwa kuwa soka na michezo mingine imefeli.

No comments:

Post a Comment