Pages

Friday, July 10, 2015

WALIMU SABA TOKA KAGERA WANYAKUA VIKOMBE VITATU NCHINI UJERUMANI


Mkoa wa Kagera umeipokea rasmi timu ya Walimu saba waliokwenda nchini Ujerumani chini ya uratibu wa shirika lisilokuwa la kiserkali la Jambo Bukoba katika mji wa Berlin
Bw. Stephen Gonzaga Meneja wa Jambo Bukoba ambaye aliongozana na timu hiyo alilielezea shirika la Discover Football kuwa linajihusisha na michezo kwa akina mama kwa dunia nzima ambapo huitisha nchi mbalimbali kushiriki kwa pamoja katika michezo ya wanawake hasa mpira wa miguu.(Kauli mbiu ya shirika hilo ni (Sports without borders and orders to women).
kushiriki michezo na kunyakua vikombe vitatu vya ushindi.
Walimu hao saba kutoka katika Halmashauri za Wilaya za Biharamulo, Bukoba Manispaa, Misenyi, Karagwe na Kyerwa, walioratibiwa na shirika la Jambo Bukoba likishirikiana na Serikali ya Mkoa wa Kagera waliondoka nchini tarehe 27/06/2015 na kuelekea nchini Ujerumani kushiriki michezo chini ya shirika lijulikanalo kama Discover Footbal na kurejea nchini tarehe 6/07/2015.
Bw. Gonzaga alisema Shirika la Jambo Bukoba lilifanikiwa kupata nafasi ya kushiriki katika michezo hiyo baada ya kukidhi vigezo kati ya nchi 400 kutoka ulimwenguni zilizoomba nafasi hiyo Tanzania ni kati ya nchi 100 zilizopata nafasi na kushiriki kwenye michezo hiyo nchini ujerumani.
Katika bara la Afrika nchi zilizofanikiwa kupeleka timu katika michezo hiyo pamoja na Tanzania ni Benin, Burkina Faso, Uganda, Rwanda, Uganda na Afrika Kusini. Nchi hizo ziliungana na nchi nyingine toka katika mabara yote na kuunda timu mbalimbali za ushindani zilizoshindana na kupata vikombe.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa Bw. Eldom Anyosisye akiipokea timu hiyo alilishukuru shirika la Jambo Bukoba kwa ushirikiano ambao umekuwepo kati yake na serikali ya mkoa wa Kagera, aidha aliwasistiza walimu hao walioshiriki michezo hiyo kutoa ujuzi na weledi walioupata katika wilaya zao hasa katika shule kwa wanafunzi.
Nao walimu walioshiriki katika michezo na kufanikiwa kupata vikombe vitatu walitoa ushuhuda wa ujuzi wa kucheza mchezo wa mpira na ujuzi mbalimbali walioupata. Pia walihaidi kutoa ujuzi huo katika Halmashauri zao hasa kwa kuwafundisha walimu wenzao na wanafunzi kwa ujumla

No comments:

Post a Comment