Pages

Friday, July 10, 2015

FIFA YAMPIGA MARUFUKU CHUCK BLAZER, KUJIHUSISHA NA SOKA

Fifa imempiga marufuku mwanachama wake wa zamani Chuck Blazer kutoshiriki katika maswala yoyote yanayohusiana na kandanda.
Blazer mwenye umri wa miaka 70 alifanya kazi kama mpelelezi na maafisa wa mashtaka nchini Marekani baada ya kukiri kuhusika na mashtaka ya kutoa hongo na ukwepaji wa kodi.
Mnamo mwezi May,maafisa kadhaa wa FIFA walikamatwa kwa mashtaka ya udanganyifu wa kutaka kupata fedha.
Taarifa ya FIFA inasema kuwa Blazer alitetekeleza vitendo vya utovu wa nidhamu.

Kwa jumla watu wapatao 14 walishtakiwa na mahakama ya Marekani ikidai walichukua hongo na kiinua mgongo fedha zilizogharimu dola milioni 150 katika kipindi cha saa 24.
Blazer alikuwa afisa wa pili mwandamizi wa FIFA kutoka kazkazini na katikati mwa Marekani na visiwa vya Carebean kuhudumu katika FIFA kutoka mwaka 1990 hadi 2011.
Akisalimiana na Blatter

No comments:

Post a Comment