Pages

Friday, July 10, 2015

MIGI, MYARWANDA MPYA WA AZAM FC AANZA KAZI CHAMAZI



 
Kiungo Myarwanda, Jen Baptiste Mugiraneza, ameanza mazoezi na klabu ya mpya ya Azam FC, leo.
Migiraneza maarufu kama Migi ameanza mazoezi na kikosi cha Azam FC chini ya Kocha Stewart Hall kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, taarifa zimeeleza, Migi bado hajamalizana na Azam FC katika suala la mkataba na huenda likafanyika leo mchana au jioni.
Kiungo huyo nyota wa APR, pia ni tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi.

No comments:

Post a Comment