Pages

Friday, July 10, 2015

KUZIONA TANZANITE, YOUNG SHE-POLOPOLO 2000/=


Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake kwenye umri chini ya miaka 20 (Tanzanite) kesho siku ya jumamosi itashuka dimbani uwanja wa Azam Complex kucheza na timu ya Taifa ya Zambia chini ya miaka 20 (Young She-Polopolo).

Viingilio vya mchezo wa kesho kati ya Tanzanite dhidi ya Young She-Polopolo ni shilingi elfu mbili (2,000/=) kwa jukwaa la mzunguko, na shilingi  elfu tatu (3,000/=) kwa Jukwaa Kuu.

Mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Wanawake za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Papua New Guinea, utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Sudan,unatarajiwa kuanza saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na kati.

Timu ya Young She-Polopolo tayari imeshwasili nchini jana jioni, na leo wakitarajiwa kufanya mazoezi mepesi leo jioni katika uwanja wa Azam Complex kw ajaili ya mchezo huo. Waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Sudan tayari wameshawasili.

Wakati huo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetoa usafiri wa mabus mawili kwa ajili ya kikundi cha ushangiliaji cha timu za Taifa (Taifa Supporters) kitachokwenda kesho Chamazi kuipa sapoti timu ya Tanzanite.

Mabasi hayo mawili yataondoka ofisi za TFF zilizopo Karume saa 6 kamili mchana kuelekea Chamazi kwa ajili ya kuishangilia timu ya Taifa ya wanawake  chini ya miaka 20 (Tanzanite).

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA     

No comments:

Post a Comment