Pages

Friday, July 17, 2015

KOCHA WA APR DUSAN SUYAGIC, AJIGAMBA KUTWAA UBINGWA WA KAGAME




KOCHA wa timu ya APR ya Rwanda, Dusan Dule Suyagic amejigamba kuwa kikosi chake kitafanya vizuri kwenye mashindano ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua kesho jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya mazoezi na timu yake yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume,  Dusan alisema msimu uliopita timu yake ilishika nafasi ya pili baada ya kufungwa na El Merreikh ya Sudan hivyo msimu huu wamekuja wakijua kuna ushindani lakini nao watahakikisha wanatoa ushindani.
“Naheshimu kila timu iliyopo kwenye mashindano haya lakini naamini APR tutaonyesha ushindani kwani lengo letu ni kutwaa ubingwa wa CECAFA”, alisema Dusan.
APR itafungua dimba la mashindano ya Kagame ambayo yanashirikisha klabu toka nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa na Al Shandy ya Sudan kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa saa 8 kabla ya Yanga na Gor Mahia kuingia dimbani saa 10.00 kumaliza ubishi wa mashabiki kuwa nani mkali kati ya hizi timu kongwe Afrika Mashariki.
Mashindano ya CECAFA yanashirikisha vilabu 13 toka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ambapo APR FC ipo kundi B pamoja na Al Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi na Hegaan FC ya Somalia.
Kundi A lina timu za Yanga na KMKM za Tanzania, Telecom ya Djibout, Gor-Mahia ya Kenya na Khartoum ya Sudan wakati kundi C lina timu za Azam ya Tanzania, Malakia ya Sudan Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.

No comments:

Post a Comment