Chicharito aliumia Jumatano iliyopita huko Houston, USA wakati wa Mechi ya Kirafiki na Honduras iliyoisha 0-0 na kutolewa nje Dakika 5 kabla Haftaimu.
Msimu uliopita, Chicharito, mwenye Miaka 27 na ambae ni Fowadi wa Manchester United, alikuwa na Real Madrid kwa Mkopo na alipaswa kurudi Old Trafford huku kukiwa na fununu za mipango ya kumuuza.
Lakini kuumia kwake na kufanyiwa operesheni iliyomwekea chuma kwenye mfupa wa begani kutamweka nje kwa Wiki 4 na hali hii itafanya mipango hiyo ya Uhamisho wake isitishwe.
Kocha wa Mexico Miguel Herrera amemwita Javier Orozco wa Klabu Bingwa ya Mexico Santos Laguna kumbadili Chicharito.
No comments:
Post a Comment