Pages

Saturday, July 11, 2015

KLABU YA STOKE CITY YASAJILI WAWILI KWA MPIGO, MARCO VAN GINKEL KWA MKOPO NA KIPA SHAY GIVEN

Stoke City wamemchukua Kiungo wa Chelsea Marco van Ginkel kwa Mkopo na pia kumsaini Kipa Mkongwe kutoka Aston Villa Shay Given lakini wamejitoa Dili ya kumchukua Fowadi wa Inter Milan, Xherdan Shaqiri.
Van Ginkel, mwenye Miaka 22, anatua Stoke kwa Mkopo wa Msimu mmoja baada ya kukosa namba huko Chelsea ambako alicheza Mechi 4 tu tangu ajiunge nao kutoka Vitesse Arnhem ya Holland Mwaka 2013.

Kipa Mkongwe Shay Given, mwenye Miaka 39, amesaini MKataba wa Miaka Miwili baada ya kuhama kama Mchezaji huru kutoka Villa.
Given, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa Republic of Ireland alieichezea Mechi 129, pamoja na Van Ginkel, wanakuwa Wachezaji wa 5 kusainiwa na Stoke City ambao wako chini ya Meneja Mark Hughes.
Wengine ni Beki Philipp Wollscheid, Kipa Jakob Haugaard na Straika Joselu.

No comments:

Post a Comment