UHAMISHO ENGLAND MPAKA SASA 2015: JAMES MILNER WA CITY ATUA LIVERPOOL, IIKAY GUNDOGAN NDANI YA MAN UNITED, FUATILIA NA WENGINE HAPA AMBAO TAYARI WAMENUNULIWA
Liverpool wameafikiana Dili ya kumsaini Kiungo wa England James Milner ambae anachezea Manchester City kwa Uhamisho wa bure.
Milner, mwenye Miaka 29, ameshakubaliana malupulupu yake binafsi na Liverpool na atajiunga rasmi nao kama Mchezaji Huru wakati Mkataba wake na City utakapomalizika hapo Julai Mosi kama akifuzu upimwaji Afya yake.
Akiwa na City kwa Miaka Mitano, Milner alifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 2, FA CUP na Kombe la Ligi, Capital One Cup.
Msimu uliopita, Milner alianza Mechi 24 na kufunga Bao 8 na kuifungia City Bao 8.
Mchezaji huyu alijiunga na City iliyokuwa chini ya Roberto Mancini Mwaka 2010 kwa Dau la Pauni Milioni 26 akitokea Aston Villa na kuichezea Klabu hiyo jumla ya Mechi 125 na kufunga Bao 18.
Klabu nyingine alizowahi kuzichezea ni Newcastle United na Klabu ya Mji wa Nyumbani kwao Leeds United ambayo alianza kucheza Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza Mwaka 2002 akiwa na Miaka 16 tu.
Klabu ya Watford yathibitisha Quique Flores kuwa Meneja wao mpya
Ilkay Gundogan
Kevin Wimmer asajiliwa na Klabu ya Tottenham Hotspurs kwa mkataba wa miaka 5
Morgan
Schneiderlin kujiunga na Klabu ya Man United baada ya kushinda mbio
hizo huku Klabu ya Arsenal nayo ikiwa kwenye mchakato huo huo wa
kumwania mchezaji huyo.
Winger wa Benfica Nicolas Gaitan nae inasemekana kujiunga na Man United
Boyata wa Man City kwenda Celtic
Luiz Gustavo anukia Old TraffordBale nae ndani ya Anga za United! lakini bado ila inasemekana wenda akajiunga Old Trafford
Post a Comment