Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini TFF, Julai 7 mwaka huu litafungua mashindano
ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 jijini Mwanza kwa mikoa yote ya
Tanzania kwa lengo la kung’amua vipaji kwa ajili ya kuunda timu ya
Taifa ya vijana wenye umri huo.
Mashindano
hayo yatakayofanyika kwa kipindi cha wiki moja, yatafanyika katika
viwanja vya CCM Kirumba na Alliance vyote vilivyopo jijini Mwanza, na
maandalizi ya michuano hiyo yamekamilika na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Mkuu wa mkoa Mwanza.
Jopo
la makocha litakua katika viwanja hivyo kusaka vipaji kwa lengo la
kuanza kuiandaa timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa miaka 13, ili
ifikapo mwaka 2019 waweze kuiwakilisha Tanzania katika fainali za Afrika
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazofanyika hapa nchini.
Mapema
wiki iliyopita Shirikisho la Soka barani Afrika - CAF liliipa Tanzania
uenyeji wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika
mwaka 2019.
TFF
katika kuhakikisha inafanya vizuri katika soka la vijana, mapema mwezi
Aprili iliendesha kozi ya waamuzi vijana jijiji Dar es salaam, ambapo
vijana 36 walishiriki kozi hiyo na kutunukiwa vyeti.
Aidha
TFF ina programu ya vijana chini ya miaka 15 ambayo ilianza kambi mwezi
Aprili mwaka huu, na inatarajiwa kucheza michezo ya kirafiki katika
mikoa saba nchini kati ya mwezi Juni na Agosti, kabla ya mwezi Disemba
kusafiri katika nchi Malawi, Zambia, Zimbabwe, Bostwana na Afrika
Kusini.
Kikosi
hicho cha umri chini ya miaka 15 kinajiandaa na kuwania kufuzu kwa
fainali za Vijana Afrika mwaka 2017 ambapo katika ziara hizo za mikoani,
walimu watatumia nafasi hiyo kungamua na kuongeza vijana wengine
katika
kikosi.
No comments:
Post a Comment