Mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling
huenda akaelekea katika klabu ya Manchester United , hata hivyo
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana wasiwasi kuhusu athari za
uhamisho huo hususani kutokana na ushindani mkali uliopo kati ya klabu
hizo mbili. Hatahivyo Liverpool imesema kuwa haiko tayari kufanya biashara na wapinzani wao wakuu kutoka Kaskazini Magharibi. Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Luois Van Gaal anavutiwa na kasi ya mchezaji huyo na uwezo wake wa kuwaponyoka mabeki. Sterling
amekataa ombi la kitita cha pauni laki moja kutoka kwa Liverpool
akisema kuwa anataka kuondoka na kukichezea kilabu ambacho kina uwezo wa
kushinda mataji.
No comments:
Post a Comment