PRINCE WILLIAM ATOA WITO KWA FIFA, ATAKA KUWEKA MASLAHI YA SOKA MBELE KWANZA
Kwenye hotuba yake kabla ya fainali ya kombe la FA nchini Uingereza, William ambaye pia ni rais wa shirikisho la soka la FA nchini Uingereza, ameilinganisha sakata ya FIFA na ile ya jiji la Salt Lake ilifyofanyika wakati Marekani ilikuwa inasaka tiketi ya kuandaa mashindano ya olimpiki ya barafu mnamo mwaka wa 2002 na kuilazimu kamati ya kimataifa ya Olimpiki kuimarika.
"Inaonekana kuna mgawanyiko mkubwa kati ya wanaocheza na kushabikia mchezo huo na madai ya ufisadi yanayowakabili wasimamizi wa mchezo huo. Alisema"
''Sawa na IOC inastahili kuonyesha ina uwezo wa kujali maslahi ya mchezo huo".
"wanaounga mkono FIFA wakiwemo wadhamini na mashirika ya jumuiya, wanastahili kuchukua jukumu la ya kushinikiza mabadiliko ndani ya FIFA.
'Iwapo hatutafanya hivyo, tutakuwa hatuwatendei haki wapenzi wa mchezo huo na mchezo wasoka kwa jumla".
Kando na hayo, Mwenyekiti wa FA, Greg Dyke, amesema kuwa Uingereza iko tayari kuunga mkono hatua ya shirikisho la soka barani ulaya UEFA kususia kombe la dunia la 2018.
Wasimazizi wa soka barani Uropa wanapanga kukutana jijini Berlin wiki ijayo kufanya maamuzi ya iwapo watasusia mchuano wa kombe la dunia la mwaka wa 2018 utakaoandaliwa Urusi au la.
Post a Comment