Pages

Tuesday, June 23, 2015

MARIO MANDZUKIC ATUA TURIN KUICHEZEA JUVENTUS TAYARI KWA VIPIMO

Juventus wamemnunua Straika wa Croatia Mario Mandzukic kutoka Atletico Madrid kwa Dau la Pauni Milioni 13.6.
Mandzukic, mwenye Miaka 29, alijiunga na Atletico Madrid mwanzoni mwa Msimu uliopita kutoka Bayern Munich na kuifungia Atletico Bao 20 katika Mechi 43.
Straika huyo mahiri amesaini Mkataba wa Miaka Minne na Ada yake huenda ikapanda hadi Pauni Milioni 15 ikiwa baadhi ya vigezo vitafikiwa.
Hii ni mara ya 3 katika Miaka Minne kwa Mandzukic kujiunga na Timu ambayo imetoka kufungwa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI kuanzia kuhamia Bayern Mwaka 2012 na Msimu uliopita Atletico na sasa Juve.
Kusainiwa kwa Mandzukic ni moja kwa moja kuthibitisha kuwa Straika wa Argentina Carlos Tevez anaechezea Juve sasa yupo njiani kujiunga tena na Timu ya kwao Boca Juniors kama Juzi alivyodokeza Lejendari wa Argentina Diego Maradona.

No comments:

Post a Comment