Pages

Tuesday, June 23, 2015

KIPA PETR CECH HUYOO NJIA NYEUPE EMIRATES, ROMAN ABRAMOVICH AMPA UHURU

Kipa wa Chelsea Petr Cech anakaribia kuhamia Arsenal kwa mujibu wa ripoti za kuaminika huko England.
Cech, mwenye Miaka 33, ameshaafikiana maslahi yake binafsi na Arsenal na kilichobaki ni kusawazisha mvutano kati ya Chelsea na Arsenal kuhusu Ada ya Uhamisho huku pande hizo mbili zikikubaliana kuendelea na mazungumzo.
Cech amebakiza Mwaka mmoja katika Mkataba wake na Chelsea na ameruhusiwa rasmi na Mmiliki wa Klabu hiyo, Roman Abramovich, kuhamia Klabu yeyote anayotaka baada ya kusugua Benchi Msimu uliopita akiwa Kipa Namba mbili nyuma ya Thibaut Courtois.

Cech alijiunga na Chelsea Mwaka 2004 akitokea Klabu ya France Rennes na kuidakia Chelsea Mechi 333. Ingawa Cech mwenyewe anapendelea kubakia London na hivyo kujiunga na Arsenal, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho hataki hilo na alipendelea Kipa huyo wa Kimataifa kutoka Czech Republic ahamie kwa Mabingwa wa France Paris Saint-Germain.
Lakini Karata ya Trufu ya Mmiliki Roman Abramovich ndiyo imemtoa kapa Jose Mourinho na kumpa mtaji Kipa Mkongwe Petr Cech.

No comments:

Post a Comment