Pages

Tuesday, June 23, 2015

MAAMUZI YA KAMATI YA UTENDAJI


Kamati ya Utendaji ya TFF imefanya kikao chake cha kawaida leo tarehe 20/06/2015 katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kisiwani Zanzibar,

Baadhi ya maamuzi yake ni haya yafuatayo:

  1. TUNZO ZA VODACOM.
Baada ya kuzingatia  mapungufu yaliyojitokeza katika uteuzi wa tuzo za ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2014/15, Kamati ya utendaji imeagiza Rais wa TFF aunde kamati maalum ya kusimamia mchakato wa utoaji wa tuzo za Vodacom. Kamati hii itazingatia umuhimu wa kuhusisha idara za ufundi za TFF katika zoezi hilo na wadhamini na ligi watahusishwa kwa ukaribu katika zoezi hili.

  1. KANUNI ZA LIGI 2015/16.
Kamati ya utendaji ilipitia rasimu ya kanuni za ligi kuu, FDL na SDL za msimu ujao wa 2015/16.
Mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kwenye maeneo yafuatayo:

  1. LESENI ZA VILABU.
Kamati ya utendaji imesisitiza kuwa hakuna klabu itakayopitishiwa usajili wake kama kupewa leseni ya klabu ya msimu.( Club Licencing).

  1. WAAMUZI.
Kamati ya utendaji imeridhia wazo la kamati ya maamuzi kuwa kuanzia msimu 2015/16 kutakuwa na jopo maalum ya waamuzi ( Elite referees) litakalochezeshwa mechi zote za ligi kuu.

Waamuzi hawa watakuwa ni 16 wa kati, 32 wa pembeni na 4 wa akiba. Hii itasaidia kuongoza ufanisi katika uamuzi. (refereeing).

  1. MGAWANYO WA MAPATO YA MILANGONI.
Vilabu vimeongezwa mgawanyo wa mapato  ya milangoni na sasa vitakuwa vinachukua asilimia 60% ya mapato ya mlangoni, makato mengine ni 18% VAT na 15% gharama za uwanja.

  1. UDHIBITI WA WACHEZAJI.
Kanuni ilikuwa inatoa fursa timu ya kuamua mechi ipi mchezaji asicheze baada ya kuwa na kadi tatu za njano imefutwa.

  1. KUSAJILI MIKATABA YA WACHEZAJI.
Kuanzia sasa mikataba kati ya wachezaji na klabu itakayotambuliwa na TFF itakuwa ni ile ambayo ni nakala halisi zilizopigwa muhuri na lakiri ya TFF  na kusajiliwa kwenye kumbukumbu ya TFF. Vilabu na mwachezaji watapewa nakala hizi baada ya  kusajiliwa na TFF.

  1. WACHEZAJI WA KIGENI.
Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu 2015/16 idadi ya wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na klabu ya ligi kuu itakuwa 7 (saba) wachezaji wote hawa, wote wataruhusiwa kucheza kwa wakati wote.

Mikakati ya kusajiliwa wachezaji hawa ni haya yafuatayo:
  1. Mchezaji awe ni mchezaji wa timu za Taifa za nchi yake ( Senior, U23, U20, U19, U17 nk) au
  2. Mchezaji awe anacheza katika ligi kuu ya nchi yake au nchi nyingine wakati anasajiliwa.

  1. Kila mchezaji wa kigeni atakayesajiliwa atalipia ada ya maendeleo. Mpira wa vijana ya dola 2,000 kwa kila msimu atakyocheza hapa nchini. Fedha hizi zitapelekwa katika mfuko wa maendeleo ya mpira (Football Development Fund).

Pia imeamriwa kuwa mikataba ya vilabu na wachezaji iliyo hai itaendelea kutambuliwa na TFF. Na kwa wale ambao tayari wapo nchini wataruhusiwa  kuuhisha (to renew) mikataba yao iwapo watakubaliana na vilabu vyao.

4. LESENI ZA MAKOCHA
Kamati ya utendaji imeamua kuwa kuanzia msimu huu, Kocha wa timu ya ligi kuu sharti awe na leseni B ya CAF au itakayolingana nayo kutoka katika mashirikisho mengine duniani na kocha msaidizi awe na leseni C ya CAF, hii ni kwa misimu mitatu.
Kuanzia msimu wa 2018/2019 kocha wa Ligi Kuu atatakiwa kuwa na leseni A ya CAF au inayolingana na hiyo kutoka katika mashirikisho mengine duniani.

Aidha Kamati ya Utendajji ya TFF imemteua Meshack Bandawe kuwa mjumbe wa bodi ya mfuko wa  maendeleo ya mpira wa miguu - TFF (FDF), Bandawe ni meneja wa PPF kanda ya ziwa.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment