Pages

Thursday, May 28, 2015

SIMBA YANYAKUWA MABEKI WAWILI KWA MPIGO

KATIKA kuimarisha safu ya ulinzi kwa msimu ujao Simba imesajili mabeki wawili, Samir Hajji Nuhu na Mohammed Fakhi jana usiku.
Wachezaji Nuhu alikuwa mchezaji wa Azam FC kwa misimu miwili amesaini mkataba wa mwaka mmoja na na  Fakhi alikuwa anachezea JKT Ruvu amesaini mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza jijini jana Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema wanatarajiwa kuona wachezaji hao wakionyesha kiwango kizuri kwa sababu wachezaji hao ni vijana wadogo.
“Mimi binafasi ni mmoja kati ya watu waliopendezewa na ukabaji wa  Fakhi lakini si hivyo, kama utakumbuka mechi yetu ya mwisho  ya ligi tulicheza na JKT Ruvu, aliisumbumbua ngome yetu hivyo baada ya mechi hata benchi la Ufundi lilimpendekeza huyu mchezaji,”amesema.
Nuhu aliwahi kuwa kuwa beki chaguo la kwanza upande wa kushoto kabla ya kuumia goti na kulazimika kuwa nje msimu mmoja lakini baada ya kupitia vipimo vyake na kujiridhisha kwamba amepona kabisa Simba wamemsajili.

Fakhi alikuwa beki tegemeo wa kati wa JKT Ruvu msimu huu na wengi walivutiwa na ukabaji wake mzuri.
Wachezaji hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Simba SC kufika watatu baada kusajiliwa kiungo wa Mbeya City, Peter Mwalyanzi kama wachezaji huru baada ya kumaliza mikataba yao katika klabu zao. 

No comments:

Post a Comment