KATIKA
kuimarisha safu ya ulinzi kwa msimu ujao Simba imesajili mabeki wawili, Samir
Hajji Nuhu na Mohammed Fakhi jana usiku.
Wachezaji Nuhu
alikuwa mchezaji wa Azam FC kwa misimu miwili amesaini mkataba wa mwaka mmoja
na na Fakhi alikuwa anachezea JKT Ruvu
amesaini mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza
jijini jana Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema
wanatarajiwa kuona wachezaji hao wakionyesha kiwango kizuri kwa sababu wachezaji
hao ni vijana wadogo.
“Mimi binafasi
ni mmoja kati ya watu waliopendezewa na ukabaji wa Fakhi lakini si hivyo, kama utakumbuka mechi
yetu ya mwisho ya ligi tulicheza na JKT Ruvu, aliisumbumbua ngome yetu hivyo
baada ya mechi hata benchi la Ufundi lilimpendekeza huyu mchezaji,”amesema.
Nuhu aliwahi
kuwa kuwa beki chaguo la kwanza upande wa kushoto kabla ya kuumia goti na
kulazimika kuwa nje msimu mmoja lakini baada ya kupitia vipimo vyake na kujiridhisha
kwamba amepona kabisa Simba wamemsajili.
Fakhi alikuwa
beki tegemeo wa kati wa JKT Ruvu msimu huu na wengi walivutiwa na ukabaji wake
mzuri.
Wachezaji hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Simba SC kufika watatu baada kusajiliwa kiungo wa Mbeya City, Peter Mwalyanzi kama wachezaji huru baada ya kumaliza mikataba yao katika klabu zao.
Wachezaji hao wanafanya idadi ya wachezaji wapya waliosajiliwa Simba SC kufika watatu baada kusajiliwa kiungo wa Mbeya City, Peter Mwalyanzi kama wachezaji huru baada ya kumaliza mikataba yao katika klabu zao.
No comments:
Post a Comment