NYOTA
wa muziki wa bongo flava nchini Diamond Platinumz amewataka wasanii wa Tanzania
kusambaza nyimbo zao kwa njia ya teknolojia ili kunufaika na jasho lao.
Diamond
aliyasema hayo wakati akizindua teknolojia ya Mziiki ili kuziingiza sokoni kazi
zake baada ya kushauriana na wadau anaoshirikiana nao kikazi ambayo pia yeye ni
balozi anayeitangaza
”Tanzania
ina wanamuziki wengi wenye vipaji lakini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
nyingi ambazo zimekuwa zikiwafanya wasifike mbali zaidi ya muziki wao kusikika
hapa nchini na wengi wao kutamba kwa muda mfupi na kupotea katika ulimwengu
hivyo watumie teknolojia hii kupeleka kazi zao sokoni ili kujikwamua”, alisema Diamond
Amesema
sababu kubwa iliyomsukuma kufanya biashara ya muziki kupitia progamu hii ni
kwamba nyimbo zake ziweze kuwafikia washabiki wake popote na muda wowote kwa
urahisi kupitia simu zao za mkononi na anakuwa na uhakika wa kupata mapato
tofauti na zinavyosambazwa na wasambazaji wa mtaani.
“Duniani kuna ushindani katika nyanja zote
hivyo sisi wanamuziki wa Tanzania tunapaswa kuhakikisha tunatoa muziki
wa viwango vya juu kuhakikisha tunalenga zaidi katika masoko ya ndani na nje kama
wenzetu wanavyofanya kusambaza kazi zao kupitia kampuni zinazotumia teknolojia
ya kisasa na kumnufaisha msanii kama ilivyo program hii ya Mziiki. Kuna umuhimu
mkubwa wa kujiamini, kufanya vizuri ili tuweze kutangaza Tanzania, kutangaza
lugha ya Kiswahili na kupata mapato ya kutosha kutokana na kazi ya muziki
ambayo ikifanywa kitaalamu inalipa kwa kiasi kikubwa” anasema Diamond
Programu ya Mziiki ambayo ilizinduliwa na Vodacom kwa kushirikiana na Spice VAS
Africa imeanza kufanya kazi na wanamuziki wa hapa nchini na nje ya nchi na
katika kipindi cha muda mfupi tayari imesajili wanamuziki wapatao 1,000 ambao
kazi zao hususani zile mpya zitasambazwa kwa njia ya kidigitali na malengo yake
makubwa ni kuhakikisha wanamuziki wanapeleka kazi zao sokoni kwa haraka na
kunufaika na jasho lao ambapo wananchi wengi wanaotumia mtandao kwenye simu zao
kupakua nyimbo wazipendazo za wanamuziki ambao wamejiunga kwenye tovuti ya
kampuni hiyo ambayo inapatikana kwa kubofya tovuti ya www.mziiki.com.
|
Pages
▼
No comments:
Post a Comment