Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
amewaagiza wasimamizi wa vituo vya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuhakikisha
sheria na taratibu zote za mechi zinafuatwa.
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) msimu huu 2014/2015 inafikia tamati kesho (Mei 9,
2015) ambapo timu zote 14 zitakuwa viwanjani katika mechi ambazo ndizo
zitakazotoa hatma ya timu zinazoshuka daraja.
Mechi
hizo zitakuwa kati ya Ndanda na Yanga (Uwanja wa Nangwanda Sijaona,
Mtwara), JKT Ruvu na Simba (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Azam na
Mgambo Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), Stand United na Ruvu
Shooting (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Kagera Sugar na Tanzania
Prisons (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Mbeya City na Polisi Morogoro
(Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Mtibwa Sugar na Coastal
Union (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
No comments:
Post a Comment