Pages

Tuesday, May 26, 2015

KIUNGO ILKAY GUNDOGAN WA BORUSSIA DORTMUN KUTUA OLD TRAFFORD

Kwa mujibu wa gazeti la Goal, kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan (pichani) amekubaliana maslahi binafsi na Manchester United tayari kwa usajili wa kwenda Old Trafford mwezi ujao. Gundogan, 24, tayari alishatangaza kuwa hatarefusha mkataba wake Dortmund lakini ada baina ya klabu hizo mbili bado haijafikiwa. Kocha wa United Louis van Gaal wiki iliyopita alikiri kuwa anatafuta kiungo mchezajishaji kwaajili ya dirisha la usajili la kiangazi. Boss huyo wa United alisema: "Namba 6 ni sehemu muhimu katika timu. "Nina maeneo mengi ntakayoboresha na namba 6 ni mojawapo."

No comments:

Post a Comment