Pages

Tuesday, May 26, 2015

WAAMUZI SASA KULIPWA 500,000 BADALA YA 250,000



KAMATI ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imepunguza idadi ya waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu na kuwaongezea posho. Imeelezwa kuwa idadi ya waamuzi itapunguzwa kutoka 90 msimu uliopita hadi kufikia 48 msimu ujao.

Aidha, posho ya waamuzi hao itaongezwa mara mbili ya mwaka jana, kutoka Sh 250,000 hadi 500,000. Akijibu maswali ya waandishi wa habari jana Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salum Chama alisema kati ya hao, waamuzi wa kati watapunguzwa kutoka 26 walioteuliwa mwaka jana, hadi kubaki 16 wakati wasaidizi watapungua kutoka 64 msimu uliopita hadi 32.

“Tumeona tupunguze idadi kupunguza changamoto, ambazo zimekuwa zikilalamikiwa lakini pia tunataka ligi yetu ichezeshwe kwa ubora wa hali ya juu,” alisema.
Chama alisema vigezo walivyotumia katika kupunguza idadi hiyo vimetokana na ripoti ya msimu uliopita, mechi  walizochezesha, uwezo na umri usiozidi miaka 45.

Alisema wanategemea baada ya kupunguza idadi hiyo ligi itachezeshwa kwa kuzingatia sheria 17 za soka na itakuwa bora zaidi na hakutakuwa na malalamiko yasio ya lazima.
Alisema nia yao ni kuhakikisha ligi inakuwa na ubora ukilinganisha na miaka iliyopita, pia kuondoa vishawishi dhidi yao.

Kuhusu posho alisema wameona waboreshe kiwango ili kutoa nafasi kwa waamuzi kuepuka vishawishi vya kupokea rushwa.
Inaendelea Uk. 31

No comments:

Post a Comment