Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki
kwa viwanja sita kutimua vumbi, michezo mitatu ikifanyika siku ya jumamosi na
michezo mingine mitatu kufanyika siku ya jumapili.
Katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, wenyeji timu ya
Polisi Morogoro watawakaribisha maafande wa Ruvu Shooting kutoka Mlandizi,
Coastal Union watakua wenyeji wa Kagera Sugar kwenye dimba la Mkwakwani, huku JKT Ruvu wakiwakaribisha Azam FC katika
uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Jumapili Mgambo JKT watakua wenyeji wa timu ya Ndanda FC
kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Mtibwa Sugar wakiwa wenyeji wa
wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika Uwanja wa Manungu Turiani.
Katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam watani wa jadi
Simba SC watakuwa wenyeji wa Young Africans, mchezo unaotarajiwa kuanza kutimua
vumbi majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment