LIGI
inayoshirikisha watoto walio chini ya umri wa miaka 16, inatarajia kuanza
kutimua vumbi kesho kutwa kwenye Uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa.
Ligi hiyo ikishirikisha timu nane za manispaa ya Iringa
na inajulikana kama Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 yenye lengo
la kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino).
Mratibu wa ligi hiyo, Haruna Salehe alisema lengo ni kukuza vipaji vya watoto na kueneza
ujumbe wa kupinga ukatili na mauaji yanayofanywa kwa walemavu wa ngozi nchini.
“Lengo ni kukuza vipaji na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wenzetu wenyewe ulemavu wa ngozi ambao wamekuwa wakiuawa kila siku jambo ambalo, hatutaki liendelee kwenye jamii yetu,”alisema.

Pia alisema mpira ni ajira na huu hauna dini, kabila wala rangi, watu wote hata watoto wanaweza kushiriki kwenye mpira hivyo tumeanzisha ligi ili kuendelea kukuza vipaji lakini tukibeba ujumbe wa kupinga ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
Alisema ligi hiyo imepata bara za shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa, ambalo watoto wameshafundishwa mafunzo ya waamuzi ambao ndio watakaochezesha ligi hiyo
No comments:
Post a Comment