Chama
cha Soka England FA, kimeanza uchunguzi kuhusu Mashabiki wa Aston Villa
kuvamia Uwanja kabla Mechi ya Uwanjani kwao Villa Park kati ya Aston
Villa na West Bromwich Albion haijamalizika na pia mara baada ya
kumalizika, Leo hii FA imetoa taarifa kuwa Kiungo wa WBA, Chris Brunt,
amefunguliwa Mashitaka kwa kutoa lugha chafu kwa Waamuzi katika Mechi
hiyo hiyo. FA
imedai kuwa Brunt alitoa lugha chafu kwa Mwamuzi mmoja wakati Mechi
imekwisha na Wachezaji wapo kwenye njia ya kuelekea Vyumba vya Kubadili
Jezi. Brunt, mwenye Miaka 30, amepewa hadi Machi 12 kujibu Mashitaka yake. Katika
Mechi hiyo ya Robo Fainali, ambayo ni Dabi ya Midlands, Villa
waliifunga WBA Bao 2-0 kwa Bao za Fabian Delph na Scott Sinclair na
kuwafikisha Nusu Fainali ya FA CUP kwa mara ya kwanza tangu 2010. Mechi
hiyo, licha ya Mashabiki kuvamia Uwanja na kusababisha isimame mwishoni
kabla haijaendelea tena na kumalizwa na Refa, ilishuhudia Kadi Nyekundu
2 kwa Mchezaji wa Villa Jack Grealish na Claudio Yacob wa WBA. Uvamizi
wa Mashabiki ulizuka tena mara baada ya Refa kumaliza Mechi hiyo na
kuleta kashikashi kubwa ambayo FA imeanza kuifanyia uchunguzi.
Kwa nini Iran iliamua kuishambulia Israel?
-
Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa kijeshi nchini Iran, shambulio hilo
lilikuwa la " kulipiza kisasi mashambulizi ya Israel dhidi ya vitongoji vya
Beirut."
GEITA GOLD YAPANDA LIGI KUU
-
Timu ya Geita Gold FC imerejea Ligi Kuu ya NBC baada ya leo kumfunga
Songea United mabao 3-1 wakiwa nyumbani Uwanja wa Nyamkumbu.
Kwa matokeo hayo Geita...
WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS
-
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen
Wasira, Leo Machi 27, 2026, Mjini Bunda Mkoa wa Mara alipokuwa akiweka
jiwe la ms...
Post a Comment