Pages

Wednesday, January 14, 2015

YAYA SANOGO ATUA CRYSTAL PALACE KWA MKOPO! ALAN PARDEW AMKARIBISHA

Crystal Palace imemsaini Straika wa Arsenal Yaya Sanogo kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu.
Sanogo, mwenye Miaka 21, anakuwa Mchezaji wa kwanza kusainiwa na Meneja mpya Alan Pardew tangu ahamie Palace kutoka Newcastle mwanzoni mwa Januari.
Ingawa Sanogo alihusishwa na kwenda kwa Mkopo kwao France Klabuni Bordeaux lakini Meneja wa Arsene Wenger alitaka kumbakisha England ili apate uzoefu zaidi wa mikikimikiki ya Ligi Kuu England.
Sanogo, ambae pia ni Mchezaji wa Timu ya Taifa ya France ya U-21, ameichezea Arsenal mara 5 Msimu huu na kufunga Bao 1 walipocheza na Borussia Dortmund kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI.

No comments:

Post a Comment