Pages

Wednesday, January 14, 2015

OUSSAMA ASSAIDI AIHAMA LIVERPOOL, ATIMKIA DUBAI AL AHLI

Winga wa Liverpool kutoka Morocco, Oussama Assaidi, mwenye Miaka 26, amehamia Al Ahli ya Dubai, Falme za Nchi za Kiarabu.
Assaidi alinunuliwa na Liverpool Mwaka 2012 kutoka Klabu ya Uholanzi Heerenveen lakini alishindwa kupata namba na kuishia kucheza Mechi 12 tu.
Msimu uliopita Assaidi alipelekwa Stoke City kwa Mkopo na kufunga Bao 5 lakini Mkopo huo sasa umefutwa na amehamia Al Ahli kwa kudumu.
Mchezaji huyo wa Morocco alikuwa Mchezaji wa 3 kusainiwa na Brendan Rodgers alipohamia Liverpool wengine wakiwa ni Fabio Borini kutoka AS Roma na Joe Allen kutoka Swansea.

Licha ya kutong’ara Liverpool, Assaidi atakumbukwa huko Stoke City baada ya kuwafungia Bao la Dakika ya mwisho la ushindi Desemba 2013 walipoichapa Chelsea 3-2.

No comments:

Post a Comment